Waziri wa Mambo ya Nje ya China azungumzia mambo nane muhimu ya kidiplomasia ya nchi hiyo katika mwaka mpya
2021-12-30 15:38:21| cri

Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi leo alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) amesema, mwaka 2022 China itatoa kipaumbele katika mambo nane ya kidiplomasia.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni kuanzisha mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China, kuunga mkono Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, kuongoza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa mambo ya kimataifa, kukabiliana na changamoto mbalimbali kufuatia janga la COVID-19, kupanua uhusiano wa wenzi wa kimataifa, kuendelea kulinda maslahi ya kimsingi ya kitaifa, kudumisha maendeleo ya China yanayofungua mlango, na kuwahudumia vizuri wananchi wa China.