WHO yaonya kutokea kwa “tsunami ya wagonjwa” wa COVID-19 aina ya Omicron na Delta
2021-12-30 09:42:05| CRI

WHO yaonya kutokea kwa “tsunami ya wagonjwa” wa COVID-19 aina ya Omicron na Delta_fororder_WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kwamba virusi vya Corona aina ya Omicron ambavyo vinaambukiza zaidi pamoja na vya Delta vinavyoendelea kusambaa vinaweza kupelekea “tsunami ya wagonjwa” na kutoa shinikizo kubwa kwenye mifumo ya afya ya taifa.

Akielezea mwitikio wa WHO tangu kutokea kwa janga la COVID-19, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ana wasiwasi mkubwa “kwa kuwa Omicron inaambukiza zaidi, na kusambaa kwa wakati mmoja na virusi vya Delta, hivyo inaweza kupelekea tsunami ya wagonjwa."

Amesisitiza kuwa janga hili linawapa na litaendelea kuwapa shinikizo kubwa watumishi wa afya ambao tayari wameshachoka pamoja na mifumo ya afya inayokaribia kudhoofika na kuharibu maisha ya watu. Na kusema shinikizo hilo halitasababisha wagonjwa wapya wa COVID-19 kuhitaji kulazwa hospitalini tu, bali hata idadi kubwa ya watumishi wa afya pia nao wataumwa.