Rais Putin na rais Biden watarajiwa kuongea kwa simu hivi karibuni
2021-12-30 09:45:17| CRI

Msemaji wa Ikulu ya rais wa Russia, Kremlin, Bw. Dmitry Peskov amesema kuwa rais wa nchi hiyo Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani Joe Biden watazungumza kwa njia ya simu katika Ikulu ya Kremlin leo Alhamisi, lakini bado hajabainisha mada za mazungumzo hayo.

Awali Rais Putin na rais Biden walizungumza kupitia video mnamo tarehe 7 mwezi Disemba wakilenga hali ya Ukraine. Baada ya mazungumzo hayo, Russia ilituma rasimu ya makubaliano kwenye Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO na rasimu ya mkataba kwa Marekani zote zikihusu uhakikisho wa usalama barani Ulaya ili nchi za Magharibi kuzingatia.