Wang Yi aeleza vipengele vitano vya diplomasia ya China katika mwaka 2021
2021-12-31 10:08:26| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana Alhamis alieleza kwa muhtasari mafanikio ya diplomasia ya China katika mwaka 2021 akitaja vipengele vitano, na kupongeza kama “kuandika ukurasa mpya wa diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa China.”

Bw Wang amefafanua kuwa kwenye masuala ya kidiplomasia, China imekusanya nguvu ya miaka 100 ya mafanikio ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), kusonga mbele kupitia ushindani na changamoto huku kukiwa na ujasiri na ushupavu, na kuandika ukurasa mpya wa diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa China.

Akitaja vipengele hivyo vitano Bw. Wang amesema kwanza, diplomasia ya mkuu wa nchi imebeba jukumu kubwa la uongozi kwenye diplomasia ya China, ambapo rais Xi Jinping aliwapigia simu mara 79 viongozi wa nchi za nje na mashirika ya kimataifa, na kushiriki kwenye shughuli kubwa za kidiplomasia zipatazo 40 kupitia njia ya video. Pili, diplomasia ya kupambana na COVID-19 imethibitisha nguvu ya China ya wajibu wa kimataifa.

Tatu diplomasia ya China kwenye maendeleo imechangia pakubwa katika harakati hizi za maendeleo duniani. Nne China imetetea haki katika diplomasia ya pande nyingi. Na tano China imetekeleza ahadi yake adhimu ya diplomasia kwa ajili ya watu, na kwamba China imefuata njia ya kuweka watu mbele, kujenga mfumo wa ulinzi kwa maslahi ya watu waliopo nje na tahadhari ya hatari na ulinzi, na imeokoa kwa mafanikio Wachina kadhaa walioshikiliwa mateka.

Kwa upande wa janga la COVID-19 Bw. Wang amesema hadi kufikia Disemaba 26 China imetoa zaidi ya dozi bilioni 2 za chanjo katika nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 120, na kuwa mtoaji mkubwa wa chanjo katika nchi za nje miongoni mwa nchi zote. Kwa mujibu wa Wang hadi sasa China imetoa barakoa bilioni 372, mavazi ya kujilinda zaidi ya bilioni 4.2 na vitendanishi zaidi ya bilioni 8.4 kwenye jamii ya kimataifa.

Mbali na hapo Bw. Wang pia ameeleza kuwa si zamani sana rais wa China Xi Jinping alitangza kuwa China itatoa dozi nyingine bilioni 1 za chanjo ya COVID-19 katika nchi za Afrika, zikiwemo dozi milioni 600 kama mchango. Ambapo amesema chanjo hizi zitazisaidia nchi za Afrika kutimiza lengo lililowekwa na Umoja wa Afrika la kuchanja asilimia 60 ya Waafrika hadi kufikia mwaka 2022.