China kuanzisha maeneo ya taifa ya mfano kuhusu mageuzi ya Tiba ya Jadi ya Kichina
2021-12-31 18:54:08| CRI

Mamlaka ya dawa za jadi za China imesema maeneo saba ya ngazi ya mkoa ya China yamepewa idhini ya kuanzisha maeneo ya taifa ya mfano kwa ajili ya mageuzi ya kina ya matibabu ya jadi ya China (TCM).

Shanghai, Zhejiang, Jiangxi, Shandong, Hunan, Guangdong na Sichuan ni maeneo saba ya kundi la kwanza kuidhinishwa. Maeneo hayo yatatangulia kwenye mageuzi katika mtindo wa huduma, maendeleo ya viwanda na usimamizi wa ubora wa dawa za jadi za kichina.