Rais Xi Jinping wa China asisitiza kujenga bandari ya biashara huria yenye ushawishi wa kimataifa
2022-04-14 11:50:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuharakisha mchakato wa kukuza mkoa wa Hainan kuwa bandari ya biashara huria ambayo ina umaalumu wa China na ushawishi wa kimataifa.  

Rais Xi alisema hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika mkoa wa Hainan, kusini mwa China, kuanzia Jumapili hadi Jumatano.

Aliagiza kufanya mageuzi ya kina na kufungua  mlango kwa pande zote, kuendelea kukuza maendeleo kwa kutegemea uvumbuzi, kufanya uratibu katika hatua za kukabiliana na COVID-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, pamoja na kuwepo uwiano kati ya maendeleo na usalama.

Rais Xi alisema kuwa Hainan utakuwa mkoa wa mfano mzuri wa kuigwa katika mageuzi na kufungua mlango katika zama mpya.