Takriban miili ya watu 106 yazikwa kufuatia mashambulizi katikati ya Nigeria
2022-04-15 09:04:21| CRI

Takriban miili ya watu 106 imezikwa hadi sasa kufuatia mashambulizi ya watu wenye silaha wasiojulikana kwenye vijiji kadhaa katikati ya Jimbo la Plateau nchini Nigeria mapema wiki hii.

Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha eneo hilo Channels Television, Dayabu Garga, afisa mkuu wa serikali ya eneo la Kanam alisema kuwa mazishi makubwa yalifanyika kwa wahanga hawa katika kaburi lisilo na kina kirefu siku ya Jumatatu, kufuatia ghasia zilizozuka siku ya Jumapili katika eneo hilo. Pia alisema bado wanatafuta maiti zaidi katika mashamba, akielezea mashambulizi hayo kuwa "ya kuangamiza."

Idadi hiyo ya watu waliouawa kwenye mashambulizi hayo ni mara ya kwanza kutajwa rasmi na serikali ambayo awali yalilaaniwa na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.