Jinsi matumizi ya lugha ya kichinia yanavyobadili maisha ya wanawake
2022-04-15 10:07:44| CRI

    Tarehe 20 ya kila mwezi April ni Siku ya Kimataifa ya lugha ya Kichina. Siku za Lugha zilizotangazwa na Umoja wa Mataifa zina lengo la kusherehekea lugha mbalimbali na tamaduni tofauti, na pia kutangaza matumizi sawa ya lugha rasmi sita zinazotumika katika Umoja huo.

    Uzuri ni kwamba, si katika Umoja wa Mataifa pekee ambapo lugha ya Kichina inatumika, bali watu wengi kutoka nchi mbalimbali wanajifunza na kupata ajira kupitia lugha hiyo. Na katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku hii ya leo, tutaangalia jinsi lugha ya Kichina inavyoendelea kupata umaarufu katika sehemu mbalimbali duniani, na jinsi matumizi ya lugha hiyo yanavyobadili maisha ya wanawake.