Tanzania yapanga kuzalisha megawati 200 za umeme kutoka joto la ardhini kabla ya mwaka 2025
2022-04-18 08:41:39| CRI

Katibu mkuu wa wizara ya nishati ya Tanzania Bw. Felchesmi Mramba, amesema Tanzania inapanga kuzalisha megawati 200 za umeme kwa kutumia joto la ardhini.

Bw. Mramba amesema hayo akiwa ziarani kwenye chanzo cha nishati hiyo huko Kiejo-Mbaka na Ngozi, mkoani Mbeya. Amesema kwa sasa Tanzania imetambua maeneo 52 yenye uwezekano wa kuwa chanzo cha nishati hiyo.

Bw. Mramba pia amesema mipango inaendelea ili kuzalisha megawati 1,100 za umeme kutoka vyanzo vya nishati endelevu vya joto la ardhini, jua na upepo kabla ya mwaka 2025. Amekumbusha kuwa Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati ya joto la ardhini, vinavyoweza kutumika kuzalisha umeme wakati vipindi virefu vya ukame vinapoathiri uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji.