China yadokeza wanaanga watakaoshiriki kwenye safari za vyombo vya anga vya Shenzhou-14 na Shenzhou-15
2022-04-18 08:33:51| CRI

Wanaanga watakaoshiriki kwenye safari za vyombo vya anga za juu vya Shenzhou-14 na Shenzhou-15 wamechaguliwa, na sasa wanafanya mazoezi na maandalizi kwa ajili ya safari hizo.

Akiongea na wanahabari, msanifu mkuu wa mfumo wa wanaanga kwenye programu ya safari za anga za juu ya China Bibi Huang Weifen, amesema wanaanga hao watakaa kwenye obiti kwa miezi sita, na wataanza kupokezana zamu kwa mara ya kwanza ili kudumisha uwepo endelevu wa wanaanga katika kituo cha anga za juu cha China.

Wanaanga sita wa vikundi viwili watakaa pamoja katika kituo cha anga za juu kwa muda wa siku tano hadi kumi.