Iran yasema Marekani inatekeleza sera ya kuchelewesha mazungumzo kuhusu suala la nyuklia
2022-04-19 09:24:55| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Saeed Khatibzad amesema Marekani inatekeleza sera ya ucheleweshaji kwenye mazungumzo kuhusu suala la nyuklia la Iran, na Iran inaisubiri Marekani kujibu pendekezo lake kuhusu kutatua masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili.

Iran na Marekani zilibadilishana taarifa kupitia mratibu wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa idara ya mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya.

Amesema Iran na pande husika za makubaliano ya  nyuklia JCPOA, zikiwemo Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Ujerumani, zimefanya kila juhudi na zinasubiri majibu mwafaka kutoka kwa Marekani ili kushughulikia masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja.