Msukosuko wa nishati nchini Kenya wapungua baada ya bei ya mafuta kupanda
2022-04-19 08:56:16| CRI

Msukosuko wa nishati uliodumu kwa wiki tatu nchini Kenya sasa umepungua baada ya mafuta kuanza kupatikana kwenye vituo vya mafuta, na serikali kupandisha bei ya mafuta.

Kuanzia tarehe 14 Aprili serikali ilipandisha bei ya dizeli na petrol kwa senti 9 dola za kimarekani mjini Nairobi, na baada ya uamuzi huo bidhaa hizo zilianza kupatiakan katika vituo vya mafuta mjini Nairobi katika maeneo ya karibu.

Mkurugenzi wa mamlaka usimamizi wa nishati na mafuta Bw. Daniel Kiptoo amesema upatikanaji wa mafuta katika nchi nzima na soko limerudi katika hali ya kawaida.

Hapo awali kaimu waziri wa nishati na mafuta wa Kenya Bibi Monica Juma, aliyalaumu mamapuni ya biashara ya mafuta kwa kufanya mafuta yaadimike, huku wakisubiri mafuta yapande bei na kupata faida zaidi.