Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ajibu maswali kuhusu kufariki kwa balozi wa Ufilipino nchini China
2022-04-19 21:52:31| CRI

Swali: Imefahamika kuwa balozi wa Ufilipino nchini China Jose Santiago L. Sta. Romana alifariki Aprili 18 nchini China. China ina maoni gani juu ya tukio hili?

Jibu: China inasikitishwa sana na kifo cha balozi Jose Santiago L. Sta. Romana. Balozi Romana alijulikana sana kwa ujuzi wake wa kina kuhusu China. Aliwahi kufanya kazi na kuishi kwa muda mrefu nchini China, na ni rafiki yetu mkubwa. Tangu aliposhika wadhifa wa balozi wa Ufilipino nchini China mwaka 2017, amekuwa akifanya kazi kwa bidii, na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya pande mbili, na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili. China imetuma salamu za rambirambi na masikitiko kwa kifo chake, na kuwapa pole kwa moyo wa dhati jamaa zake. Tutashirikiana na familia ya balozi Romana na Ubalozi wa Ufilipino nchini China kushughulikia ipasavyo mambo yanayohusika, na kutoa huduma zinazohusika kadiri tuwezavyo.