Benki ya dunia yakadiria msukosuko wa madeni utaendelea kuwa mbaya mwaka huu
2022-04-19 08:57:38| CRI

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass amesema kufuatia kuwepo kwa deni kubwa na nakisi kubwa, nchi mbalimbali duniani ziko kwenye shinikizo kubwa la kifedha, na msukosuko wa madeni kwa mwaka huu unakadiriwa kuendelea kuwa mkubwa.

Akiongea mjini Washington kwenye mkutano wa pamoja kati ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Bw. Malpass amesema madeni ni moja ya matatizo mawili makubwa yanayolikabili ongezeko la uchumi wa dunia, na kwamba asilimia 60 ya nchi zenye mapato ya chini tayari ziko kwenye msukosuko wa madeni au zina hatari kubwa ya kuwa kwenye msukosuko huo.

Ametaja tatizo la pili kubwa ni mfumuko wa bei ambao pia unaleta changamoto kubwa, na kusema sera zinatakiwa kurekebishwa ili kuhimiza upatikanaji wa bidhaa, na sio kuchochea mahitaji peke yake.