Watu tisa wajeruhiwa baada ya jengo la bunge Somalia kushambuliwa kwa mizinga
2022-04-19 08:45:44| CRI

Watu wasiopungua tisa wamejeruhiwa baada ya jengo la bunge la Somalia kushambuliwa kwa mizinga, ambako wabunge wateule walikuwa mkutanoni.

Ofisa wa polisi aliyekuwa katika eneo la tukio amesema walinzi wawili wa kiongozi wa upinzani ni miongoni mwa majeruhi waliokuwa katika Villa Hargeisa, iliyoko ndani ya Ikulu mjini Mogadishu.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, shambulizi hilo lilitokea wakati wabunge wateule wakiwa kwenye mkutano kuhusu uchaguzi ujao wa maspika na makamu wao wa mabaraza mawili ya bunge.

Kundi la Al-Shabab ambalo limeongeza mashambulizi ili kuvuruga uchaguzi, limetangaza kuwajibika na shambulizi hilo.