Watanzania wahimizwa kujifunza lugha ya Kichina kama daraja la kupata fursa
2022-04-20 08:46:43| CRI

Serikali ya Tanzania imewahimiza wananchi kujifunza lugha ya Kichina ambayo imeitaja kama daraja la kupata fursa, ikiwemo ajira.

Naibu waziri wa habari, mawasiliano na Tehama Bw. Kundo Mathew amesema kujifunza lugha ya Kichina kunatoa fursa za ajira katika kampuni za China nchini Tanzania.

Akiongea kwenye maadhimisho ya Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika katika ubalozi wa China nchini Tanzania, Bw. Mathew ameeleza matarajio yake kwa wanafunzi vijana wa Tanzania wanaojifunza lugha ya Kichina, akitumai watapata fursa ya kuendeleza masomo yao nchini China, na kutumikia nchi kwa uwezo halisi baada ya kuhitimu.