Rais Xi ahimiza ujenzi wa serikali mtandao na mageuzi ya kifedha
2022-04-20 09:03:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China amehimiza juhudi kwenye ujenzi wa serikali mtandao na kuendeleza mageuzi kwenye mfumo wa mambo ya fedha kwenye ngazi ya mkoa na chini yake.

Rais Xi amesema hayo kwenye mkutano wa 25 wa kamati kuu ya chama unaohusu kuimarisha mageuzi. Mkutano huo umepitia na kupitisha hatua mbalimbali kuhusu mambo ya serikali mtandao, na kuanzisha mfumo wa kigezo cha ukaguzi kwa maofisa wanaomaliza muda wao, kwenye masuala ya usimamizi wa maliasili, na kuhimiza utaratibu wa kutoa motisha kwa jumuiya ya watafiti wa kisayansi, pamoja na mpango wa utendaji kazi kuhusu uungaji mkono wa kifedha kwenye mambo ya uvumbuzi.

Rais Xi pia amesisitiza juhudi zifanyike kutekeleza kikamilifu mkakati wa kitaifa wa kuimarisha mtandao wa internet wa China, na kutoa mwito wa matumizi mapana ya teknolojia za kidigitali kwenye mambo ya usimamizi wa serikali na utoaji wa huduma.