Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito kwa Russia na Ukraine kusitisha mapigano wakati wa Pasaka
2022-04-20 09:25:33| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa Russia na Ukraine kusitisha mapigano kwa siku nne kwa ajili ya kutolewa kwa misaada ya kibinadamu wakati wa Pasaka.

Bw. Guterres alipokutana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, amesema Umoja wa Mataifa unapanga kupeleka msafara wa misaada ya kibinadamu kwenye maeneo ya Mariupol, Kherson, Donetsk na Luhansk. Russia na Ukraine zinatakiwa kusitisha mapigano kuanzia tarehe 21 hadi 24, ili raia wanaotaka kuondoka waondoke kwa usalama na kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia walioko kwenye sehemu zilizoathiriwa zaidi na mapigano hayo.

Ameongeza kuwa hadi sasa watu zaidi ya milioni 12 nchini Ukraine wanahitaji misaada ya kibinadamu na idadi hiyo huenda ikaongezeka hadi milioni 15.7.