Chai ya kichina yakutana na mwinyo wa Afrika Kusini katika Siku ya Lugha ya Kichina
2022-04-20 08:47:21| CRI

Ushirikiano wa kielimu kati ya China na Afrika Kusini umeleta utamaduni wa chai ya kichina kwenye shamba la mwinyo la Groot Constantia mjini Cape Town, lenye historia ndefu zaidi nchini Afrika Kusini, ili kuhimiza mawasiliano ya kiutamaduni na kusherehekea Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa Aprili 20 kila mwaka.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucious ya Dawa ya Kichina katika Chuo kikuu cha Western Cape Zeng Liren amesema,  utengenezaji wa chai ya kichina na mwinyo unahitaji vitu vinavyofanana ambavyo ni moyo wa kujitolea, uchapaji kazi na ufundi wa juu, kwa hivyo taasisi yake imeandaa shughuli hiyo ya chai kwenye shamba la mwinyo ili kuhimiza mawasiliano kati ya tamaduni hizo mbili.