Idadi ya watu wanaokumbwa na njaa pembe ya Afrika huenda ikaongezeka hadi milioni 20 mwishoni mwa mwaka
2022-04-20 09:25:06| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema ukame na mgogoro wa Ukraine vinaweza kuongeza idadi ya watu wanaokumbwa na baa la njaa katika pembe ya Afrika kutoka milioni 14 hadi kufikia milioni 20 ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Bw. Dujarric amesema katika kipindi cha miezi sita ijayo, Shirika la mpango la chakula la Umoja wa Mataifa WFP litahitaji dola za kimarekani milioni 473 kuongeza misaada na kuokoa maisha ya watu nchini Ethiopia, Kenya na Somalia.