Rais wa China ahutubia ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Asia la Bo’ao
2022-04-21 10:47:44| CRI

Mkutano wa mwaka 2022 wa Baraza la Asia la Bo’ao umefunguliwa huko Bo’ao mkoani Hainan, China.

Rais Xi Jinping wa China amehutubia ufunguzi wa mkutano huo, akihimiza nchi mbalimbali duniani kushirikiana ili kukabiliana na changamoto, na kuanzisha mustakabali mzuri.

Rais Xi amesema hivi sasa mabadiliko ya dunia, zama na historia yanatokea kwa njia ambayo haijawahi kuonekana, na kuleta changamoto zinazopaswa kuzingatiwa na binadamu. Amesisitiza kuwa, nguvu kubwa zaidi ya kukabiliana na changamoto hizo ni mshikamano, na nchi mbalimbali duniani zinapaswa kufuata mkondo wa zama wa amani, maendeleo, ushirikiano na mafanikio ya pamoja, na kushirikiana ili kukabiliana na changamoto.