UM nchini Ethiopia waadhimisha siku ya lugha ya kichina na kutoa mwito wa mafungamano ya utamaduni na lugha
2022-04-21 09:15:59| CRI

Watumishi wa Umoja wa mataifa nchini Ethiopia jana waliadhimisha siku ya kimataifa ya lugha ya kichina kwa lengo la kueneza mafungamano ya utamaduni na lugha. Maadhimisho hayo yameandaliwa kwa pamoja na Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA na ujumbe wa China kwenye umoja wa Afrika, lakini kutokana na tahadhari za janga la COVID-19 maadhimisho hayo yalifanyika kwa njia ya video.

Ofisa mwandamizi wa UNECA Bw. Oliver Chinganya amesema maadhimisho hayo ni siku muhimu kwa Umoja wa mataifa kuhimiza mambo ya pande nyingi, kuwepo kwa tamaduni mbalimbali, na matumizi ya moja kati ya lugha sita rasmi za Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Chen Xufeng, amesema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya lugha ya Kichina duniani, nchi 16 za Afrika zimeiweka lugha ya kichina kwenye mitaala yao.