Rais Xi Jinping ajibu barua kutoka wanafunzi wa Uingereza kuhusu mabadiliko ya tabianchi
2022-04-22 08:26:45| CRI

Rais Xi Jinping wa China amejibu barua kutoka wanafunzi wa shule ya msingi ya Francis Holland nchini Uingereza kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.


Kwenye barua yake, rais Xi amebainisha kuwa Dunia ni familia kubwa, na binadamu wote wanatoka jumuiya moja, akisema wakati mabadiliko ya tabianchi yakileta  changamoto kwa binadamu wote, ushirikiano unahitajika ili kutatua suala hilo.


Rais Xi amesisitiza kuwa China inaheshimu na kupenda mazingira ya asili tangu enzi na dahari. Amesema China inatoa wito kwa jamii nzima kulinda na kuhifadhi mazingira kama watu wanavyotunza macho yao, na kujituma katika kusukuma mbele maendeleo ya kijani ili kuijenga China iwe nchi inayopendeza.