Msomi wa Nigeria: Kuiteka nyara dunia kwa mgogoro wa Ukraine kunaonesha siasa ya umwamba ya nchi za magharibi
2022-04-22 11:04:27| CRI

Wakati athari za mgogoro kati ya Russia na Ukraine zinazidi kuenea duniani, sauti nyingi zaidi zenye mantiki zimeanza kusikika kwenye jamii ya kimataifa. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa China ya Nigeria Bw. Onunaiju Charles Okechukwu hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, alisema baadhi ya nchi za magharibi zimekuwa zikijaribu kuiteka nyara dunia kwa kutumia mgogoro wa Ukraine, na kuzilazimisha China na nchi za Afrika kuchagua upande moja kwenye suala hilo, hali inayoonesha mara nyingine tena siasa ya umwamba ya nchi za magharibi. Amesisitiza kuwa hatua hiyo si kama tu haisaidii kutatua mgogoro, na bali inaweza kuuchochea.