Mashambulizi mawili nchini Afghanistan yasababisha vifo na majeruhi
2022-04-22 09:14:38| CRI

Mashambulizi mawili yaliyotokea jana nchini Afghanistan yamesababisha vifo na majeraha kwa makumi ya watu.

Ofisa mwandamizi wa mkoa wa Balkh, kaskazini mwa nchi hiyo amesema shambulizi dhidi ya msikiti mmoja huko mji wa Mazar-i-Sharif, mkoani humo limesababisha vifo 10 na majeruhi 15. Shuhuda mmoja amesema wakati shambulizi linatokea kulikuwa na watu wengi wakifanya ibada msikitini. Ripoti kutoka shirika la habari la nchi hiyo iliyomnukuu mkuu wa hospitali moja mjini Mazar-i-Sharif, idadi hizo zinaweza kuwa kubwa zaidi.

Shambulizi lingine limetokea katika mji mkuu wa mkoa wa Kunduz baada ya basi lililobeba wanajeshi kukanyaga mabomu yaliyotegwa kando ya barabara na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine 22 kujeruhiwa. Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na mashambulizi hayo.