Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki afariki dunia
2022-04-22 18:49:25| cri


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo ametangaza kuwa aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90. 

Akilihutubia taifa kwa njia ya televisheni, Rais Kenyatta amemtaja Bw. Kibaki kuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake kuhudumia wakenya, na aliyefanya kazi kwa bidii kufanya mengi kwa ajili ya nchi yake.