Thamani ya biashara kati ya China na Afrika yaweka rekodi mpya mwaka 2021
2022-04-25 14:03:37| CRI

Tamasha la Nne la Mauzo ya Bidhaa za Afrika Mtandaoni litafanyika kuanzia Aprili 28 hadi Mei 12. Takwimu zimeonesha kuwa, idadi ya makampuni yanayoshughulikia biashara ya mtandaoni (E-commerce) yatakayoshiriki katika tamasha hili itazidi 300, idadi ya chapa za bidhaa itazidi laki moja, na idadi ya wafanyabiashara itazidi milioni 1. Shughuli hii itaongeza msukumo wa kukabiliana na janga la COVID-19 na kuhuisha uwezo wa matumizi.

Mkurugenzi wa Idara ya biashara ya kielektroniki na TEHAMA katika Wizara ya Biashara Qian Fangli ameeleza kuwa, Mikoa ya Hunan, Zhejiang, Hubei na Hunan italeta bidhaa zenye umaalumu wa kiafrika kutoka nchi 23 za Afrika zikiwemo kahawa ya Ethiopia, mchuzi wa pilipili ya Rwanda na chai nyeusi ya Kenya kupitia matangazo ya moja kwa moja ya mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China na watangazaji wa Afrika, na wateja watapata fursa ya kushuhudia mtindo wa kipekee wa Afrika.

Katika miaka ya hivi karibuni, biashara ya mtandaoni imekuwa ikikua kwa kasi barani Afrika, ambapo makampuni ya Afrika na watu binafsi wana hamu ya kujifunza kutokana na uzoefu wa China katika nyanja ya dijitali, na kuimarisha ushirikiano. Naibu mkurugenzi wa Idara ya mambo ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhou Ping ameeleza kuwa katika mwaka 2021, thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 35.3, na kuweka rekodi mpya katika historia.