Zaidi ya watu 100 wafariki katika mlipuko uliotokea kwenye kiwanda haramu cha kusafisha mafuta nchini Nigeria
2022-04-25 08:36:32| cri

Watu zaidi ya 100 wamefariki katika mlipuko uliotokea kwenye kiwanda haramu cha kusafisha mafuta katika mpaka kati ya majimbo ya Imo na Rivers kusini mwa Nigeria.

Habari zinasema, kiwanda hicho haramu hupokea na kutengeneza mafuta ghafi ambayo huibwa na magenge haramu kutoka mabomba ya mafuta. Serikali ya jimbo la Imo inamsaka mmiliki wa kiwanda hicho, na kuanza kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.