Ushirikiano wa usalama kati ya China na Visiwa vya Solomon uko ndani ya maeneo ya mamlaka ya nchi hizo mbili
2022-04-26 13:08:53| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema, ushirikiano wa usalama kati ya China na Visiwa vya Solomon umeanzishwa juu ya msingi wa usawa na kunufaishana. Ushirikiano huo uko ndani ya maeneo ya mamlaka ya nchi hizo mbili, huku ukifuata sheria na desturi za kimataifa.

Bw. Wang amesema hayo katika mkutano na wanahabari baada ya waziri mkuu wa Australia Scott Morrison kusema kwamba kituo cha kijeshi cha China katika Visiwa vya Solomon kitakuwa mstari mwekundu kwa serikali yake.

Bw. Wang ameeleza kuwa ushirikiano huo ni wa wazi, haki, halali na usiolaumiwa. Tetesi kwamba China itajenga kituo cha kijeshi katika Visiwa vya Solomon ni za uwongo mtupu uliotungwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya.