China na nchi za Afrika zinazotumia lugha ya Kifaransa zafanya semina ya mtandaoni kuhusu demokrasia
2022-04-27 09:05:05| CRI

China na nchi 22 zinazotumia lugha ya Kifaransa barani Afrika zimefanya semina ya mtandaoni yenye mada ya “utafiti na utekelezaji wa demokrasia katika vyombo vya utungaji wa sheria vya China na Afrika.”


Naibu spika mkuu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC) Ding Zhongli, amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa semina hiyo ya siku mbili, akisema moyo wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika umejenga undugu usioweza kuvunjika. Pia umeleta uhusiano wa wenzi wa kushirikiana kwa karibu kati ya pande hizo mbili, na utaanzisha mustakabali mzuri kwa jumuiya ya China na Afrika yenye musktakabali wa pamoja katika  zama mpya.


Ding amesema Bunge la Umma la China liko tayari kushirikiana na mabunge ya Afrika kuchangia kupatikana kwa demokrasia kweli na nzuri, kuendelea kuboresha ustawi wa watu, na kuhimiza demokrasia katika uhusiano wa kimataifa.