Rais wa China ahimiza kujenga mfumo wa kisasa wa miundombinu
2022-04-27 10:59:00| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kufanya juhudi za kuimarisha ujenzi wa miundombinu katika ujenzi wa mfumo wa kisasa wa miundombinu nchini.

Rais Xi amesema hayo katika kikao cha 11 cha Kamati Kuu ya Mambo ya Fedha na Uchumi inayoongozwa naye.

Rais Xi amesema, miundombinu ni nguzo ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, akiihimiza nchi kuratibu maendeleo na usalama, na kuboresha mpangilio, muundo, kazi na mitindo ya maendeleo ya miundombinu.

Kwa mujibu wa kikao hicho, kuimarisha ujenzi wa miundombinu kwa pande zote kuna umuhimu mkubwa katika kuhakikisha usalama wa taifa, kurahisisha mzunguko wa ndani na mizunguko ya pande mbili ya masoko ya ndani na nje, kupanua mahitaji ya ndani na kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu.