Putin: Russia yatarajia kufikia makubaliano na Ukraine kwa njia ya kidiplomasia
2022-04-27 08:43:43| cri


 

Rais wa Russia Vladimir Putin amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana mjini Moscow na kusema, Russia iko tayari kufanya mazungumzo na Ukraine na kutarajia kufikia makubaliano kupitia njia za kidiplomasia.

Rais Putin pia alisema, Russia daima imekuwa ikiunga mkono Umoja huo, na kuunga mkono kikamilifu kanuni ambazo Umoja wa Mataifa umetegemea, na itaendelea kufanya hivyo katika siku zijazo.