CGTN yapata tuzo ya Dhahabu katika Tuzo za Televisheni na Filamu za New York 2022
2022-04-28 15:13:30| CRI

Washindi wa tuzo za televisheni na filamu za New York kwa mwaka 2022 walitangazwa Aprili 26 katika hafla ya kawaida ya tamasha wasimulizi wa hadithi. Video maalum ya muziki ya mwaka mpya ya CGTN inayoitwa "A Musical Toast to 2022" imepata medali ya dhahabu katika kitengo Maalum cha Sanaa za uigizaji. CGTN pia imetunukiwa tuzo mbili za fedha na tatu za shaba katika vipengele vingine.

Maingizo ya filamu na televisheni toka kwa watengenezaji filamu na wasimulizi wa hadithi kutoka nchi na maeneo 42 yalipigiwa kura mtandaoni. Maingizo yote katika shindano la mwaka huu yalifanyiwa maamuzi mtandaoni na kukaguliwa na majaji zaidi ya 200 wa tamasha hilo wakiwa ni watayarishaji, waongozaji, waandishi na wataalamu wengine wa ubunifu wa mambo ya habari kutoka kote duniani.

Video hiyo ya mwaka mpya ilikusanya wanamuziki kutoka duniani kote, ambao walituma salamu zao za heri kwa kuimba wimbo maarufu wa Kichina kwa kutumia ala zao. Wimbo wa asilini kwenye video hiyo ulitungwa na mwanamuziki mashuhuri wa China, Shi Wanchun.