China yaitaka jumuiya ya kimataifa kuzisaidia nchi za Maziwa Makuu kukabiliana na changamoto
2022-04-28 10:00:02| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amehutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, akiitaka jumuiya ya kimataifa kuzisaidia nchi za eneo la Maziwa Makuu kukabiliana na changamoto.


Balozi Zhang amesema hivi sasa katika eneo hilo mawasiliano ya kidiplomasia yanafanyika mara kwa mara, hali ya kuaminiana imeimarishwa, na ushirikiano wa kikanda umezidishwa. Hata hivyo, amesema hali ya usalama katika eneo hilo bado ni tete, haswa vitendo vya kimabavu vya makundi yenye silaha vinashamiri katika sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuongezwa kuwa matatizo ya muda mrefu yanayoathiri amani na maendeleo ya eneo hilo yanapaswa kuzingatiwa.


Balozi Zhang amesema, China itatoa msaada kwa Ofisi ya Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Maziwa Makuu, na pia itaendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za eneo hilo na za mashirika ya kikanda, na kuunga mkono juhudi zao za kutimiza amani, usalama na maendeleo.