Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapongeza juhudi za kidiplomasia katika eneo la Maziwa Makuu
2022-04-29 10:57:46| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepongeza kuimarishwa kwa diplomasia ya kikanda katika eneo la Maziwa Makuu, huku likielezea wasiwasi juu ya vitendo vya kimabavu vya makundi yenye silaha.

Katika taarifa yake, nchi wajumbe wa Baraza hilo wamepongeza juhudi za kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili na pande nyingi. Wakati huo huo, wameeleza wasiwasi wao mkubwa kuhusu mzozo wa kibinadamu katika sehemu ya mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unaochangiwa na ukosefu wa usalama na vitendo vya kimabavu vya vikundi vyenye silaha.

Wamelaani makundi yote yenye silaha yanayofanya vurugu nchini DRC na katika nchi nyingine za eneo hilo, na kuyataka yaweke silaha chini mara moja.