Bidhaa za Afrika zakaribishwa na wateja wa China
2022-04-29 10:01:14| cri


Tamasha la nne la manunuzi ya bidhaa za Afrika limezinduliwa jana kwenye mtandao, ambapo bidhaa nyingi za mvinyo, kahawa, matunda na kadhalika kutoka Afrika zinawafikia wateja wa China kupitia manunuzi ya mtandaoni.

Hii ni mara ya tatu kwa tamasha hilo kufanyika tangumwaka 2019, na limevutia makampuni na wateja wengi. Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zimeonyesha kuwa, thamani ya mauzo kutokana na tamasha la mwaka 2021 ilifikia dola za kimarekani bilioni 105.6 ndani ya siku 15.

Habari zinasema, katika tamasha la mwaka huu, bidhaa za mvinyo, kahawa, juisi na kadhalika kutoka Afrika Kusini, Tanzania, Rwanda, Benin, Cabo Verde zitaonyeshwa kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye mtandao.