Watu 132 wafariki kutokana na surua nchini Jamhuri ya Kongo
2022-04-29 09:59:00| cri

Waziri wa Afya nchini Jamhuri ya Kongo, Gilbert Mokoki amesema, watu 132 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Surua nchini humo.

Waziri huyo amesema, mkoa wa Ponte-Noire ni kiini cha janga hilo, ukiwa na kesi 5,488 zilizoripotiwa, pamoja na vifo 112 tangu mwaka huu uanze.

Mokoki amesema, Serikali ya Jamhuri ya Kongo imechukua hatua zote zinazotakiwa kuimarisha ufuatiliaji wa janga hilo na utoaji wa chanjo zinazotakiwa, na kutaka watu kupata huduma za afya mara wanaohisi kuwa na dalili za ugonjwa huo.