Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu nchini Pakistan
2022-04-29 09:48:05| cri


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limelaani shambulizi la kigaidi kwenye basi la abiria la Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Karachi nchini Pakistan lililotokea jumanne wiki hii.

Wajumbe wa Baraza hilo wamelaani vikali shambulizi hilo lililosababisha vifo vya raia watatu wa China na mmoja wa Pakistani na kuwajeruhi wengine wengi.

Baraza la usalama limetoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali za China na Pakistan, na kusisitiza kuwa inapaswa kuwaadhabu wanaopanga, wafadhili na watu wanaofanya mashambulizi hayo ya kigaidi