Msalaba Mwekundu unavyosaidia kukwamua shida za wanawake
2022-05-06 08:00:00| CRI

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali nyekundu ni shirika la kibidamu, ambalo lina wahudumu wa kujitolea wapatao takriban milioni 97 kote duniani. Shirika hili lilianzishwa kwa maslahi ya afya ya binadamu ikiwemo kuzuia na kupunguza mateso kwa binadamu bila ubaguzi wowote kwa misingi ya kitaifa, rangi, jinsia, imani za dini, daraja la kijamii au hata maoni ya kisiasa.

Kila ifikapo tarehe 8 ya mwezi Mei, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali nyekundu linaadhimisha siku yake duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu yaani “Kuwa Binadamu” inakumbusha watu kuwa na moyo wa kiungwana na kuwafanyia ukarimu watu wengine. Baadhi ya wakati, sisi kama binadamu tunahitaji kukumbushwa kidogo kwamba sote tuko sawa, na hatuna tofauti na wengine.

Kwa kaulimbiu yake "Sisi Sote ni Binadamu", ambayo inahimiza watu kuwa wema na huruma kwa wengine, kwani kufanya vitendo vidogo tu vya wema vinaweza kusaidia sana katika kutoa tumaini kwa watu wenye uhitaji mkubwa wa msaada, haswa wakati wa dhiki na shida. Mbali na mjukumu mengine, shirika hili pia linatupia jicho shida mbalimbali za wanawake. Hivyo leo hii katika Ukumbi wa Wanawake tutaangalia Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali nyekundu linavyosaidia kukwamua shida za wanawake.