Mei Mosi, ni Siku ya Wafanyakazi Duniani. Katika kuadhimisha siku hii, wafanyakazi huandamana kwa amani, na kuwasilisha madai ama malalamiko yao kwa viongozi husika, na kutarajia majibu ya malalamiko yao. Katika kipindi cha wanawake cha leo, tutazungumzia jinsi wanawake wanavyotumia nafasi zao katika kutimiza majukumu yao na pia kutoa mchango wao katika jamii.