Rais Xi Jinping atoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki
2022-05-01 19:24:52| cri

Rais Xi Jinping wa China tarehe 28 Aprili alitoa salamu za rambirambi kwa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kufuatia kufariki dunia kwa rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki. Kwenye salamu hizo, rais Xi alitoa maombolezo makubwa kutokana na kifo cha marehemu Kibaki, na kutoa pole kwa familia ya marehemu Kibaki.

Kwenye salamu hizo, rais Xi alimsifu marehemu Kibaki kuwa kiongozi hodari wa Kenya na rafiki mkubwa wa watu wa China ambaye alitoa mchango muhimu kwa kukuza uhusiano kati ya China na Kenya. Aliongeza kuwa, China inatilia maanani uhusiano kati yake na Kenya, ingependa kufanya bidii pamoja na Kenya ili uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakakti kwa pande zote kati ya China na Kenya uendelee kunufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.