Kenya yaongeza mshahara kwa asilimia 12 kufuatia athari za uchumi
2022-05-02 10:12:34| CRI

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana alitangaza kuongeza mara moja mshahara ambao ni asilimia 12 kwa kiwango cha chini, wakati alipohudhuria kwenye sherehe ya wafanyakazi jijini Nairobi.

Kenyatta amesema uamuzi wa kuongeza mshahara unalenga kuwakwamua wafanyakazi kwenye gharama zinazoongezeka za maisha na kuhakikisha ushindani wa kiuchumi. Kiongozi huyo amesema kwa miaka mitatu sasa wafanyakazi hawajaongezewa mshahara na gharama za maisha zinaendelea kuongezeka, huku mfumuko wa bei ukiwa kati ya asilimia tano na sita hivi karibuni, hivyo serikali imeonelea ni muhimu kuongeza mshahara wa kiwango cha chini. Kenyatta amewataka viongozi kurekebisha viwango hivyo ili kulinda ustawi wa wafanyakazi.

Mara ya mwisho Kenya kuongeza mshahara ilikuwa ni mwaka 2018 wakati Kenyatta alipotangaza ongezeko la asilimia tano.