Kenya yasema kanuni kali zinaweza kuumiza usafirishaji wa maua katika Umoja wa Ulaya
2022-05-03 09:43:00| CRI

Umoja wa Ulaya umeanzisha kanuni kali ambazo zinawahitaji wakulima wa maua wa Kenya kupunguza kiwango cha mbolea, dawa za kuua wadudu na maji yanayotumika katika uzalishaji, hivyo kufanya bidhaa hiyo ififie kwenye umoja huo.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Baraza la Biashara ya Maua la Kenya (KFC), Clement Tulezi amesema kanuni mpya ni tishio kwa uzalishaji, huku wadau wakionya kwamba suala hili linaweza kuleta athari tofauti kwenye ubora na kiwango cha bidhaa. Tulezi ameongeza kuwa kanuni hizo zitarejesha nyuma hatua zinazochukuliwa dhidi ya wadudu waharibifu na magonjwa pamoja na kupunguza mbolea kwenye udongo kwa kuwa matumizi ya mbolea yatakuwa na kiwango maalumu.

Naye Jack Kneppers, mlimaji mkubwa wa maua wa Naivasha, amekiri kwamba gharama kubwa za mafuta, umeme na kusafirisha mzigo zinaweza kudhoofisha ukuaji wa sekta, na kwamba bidhaa zilikuwa na faida ndogo katika soko la Ulaya licha ya gharama kubwa za uzalishaji.