Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani mashambulizi yanayoendelea kulenga raia nchini Afghanistan
2022-05-04 10:51:09| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yanayoendelea ambayo yanawalenga raia nchini Afghanistan.

Baraza hilo lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kulaani mashambulizi hayo, likiwemo shambulio dhidi ya msikiti wa Mawlawi Sekander huko Kunduz Aprili 22 na kuua zaidi ya watu 25, na shambulio dhidi ya msikiti wa Khalifa Sahib huko Kabul Aprili 29, ambapo takriban watu 30 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo yalifuatia mashambulizi mengine kadhaa ya hivi majuzi dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na jamii za watu wachache ambao ni waumini wa dini kote nchini Afghanistan wakati wa mwezi wa Ramadhani.

Taarifa hiyo ilisema, wajumbe wa Baraza la Usalama wamesisitiza tena kwamba ugaidi wa aina zote ni moja ya vitisho vikali kwa amani na usalama wa kimataifa.