Xi Jinping awahamasisha vijana kuchangia zaidi kwenye sekta ya anga ya juu ya China
2022-05-04 10:45:28| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewahamasisha vijana waliopo kwenye sekta ya anga ya juu kutoa mchango zaidi kwenye sekta ya utafitiwa anga ya juu na kutimiza uwezo wa kujitegemea zaidi kupitia uvumbuzi kwenye sekta ya sayansi na teknolojia ya anga ya juu ya China.

Rais Xi ameyasema hayo Jumatatu kwenye barua aliyoituma kwa timu ya vijana ya ujenzi wa kituo cha anga ya juu kwenye Shirika la Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu la China (CASC) kabla ya Mei 4 ambayo ni Siku ya Vijana ya China. Rais Xi amesema mambo ya anga ya juu ya China yanazidi kupata maendeleo mapya, na vijana wengi kwenye sekta hiyo wamefanya kazi ya uongozi wakibeba majukumu muhimu, ambao wameonyesha  ujasiri wa vijana wa China wa kusonga mbele katika zama mpya.