Mahakama kuu ya Marekani kuanzisha uchunguzi juu ya kuvuja kwa rasimu ya maoni kuhusu haki za utoaji mimba
2022-05-04 10:50:05| CRI

Mahakama kuu ya Marekani itaanzisha uchunguzi juu ya kuvuja kwa rasimu ya maoni kuhusu haki za utoaji mimba.

Kwenye taarifa iliyotolewa jana Jumanne, Jaji Mkuu John Roberts amethibitisha uhalali wa waraka unaoonesha kuwa majaji wengi walikuwa tayari kupindua kesi ya kihistoria ya mwaka 1973 ya Roe V. Wade ambayo ilihalalisha utoaji mimba kote nchini.

Roberts amesisitiza kuwa rasimu hiyo “haiwakilishi uamuzi wa Mahakama au msimamo wa mwisho wa mwanachama yeyote kuhusu masuala ya kesi hii.”

Ameendelea kusema kuwa usaliti huu wa siri za mahakama uliokusudia kudhoofisha shughuli za Mahakama hautafanikiwa, na kazi ya Mahakama haitaathirika kwa njia yoyote.

Waraka uliovuja ulichapishwa na Politico Jumatatu usiku, ambao utaondoa kabisa ulinzi wa utoaji mimba katika ngazi ya Serikali kuu na kuyapa mamlaka majimbo mbalimbali.