Rais wa Tanzania awahimiza wananchi kutoacha kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona
2022-05-05 10:36:02| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania jana aliwahimiza wananchi kutoacha kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya janga la Corona, kwa kuwa ugonjwa huo bado ni tishio kwa binadamu.

Rais Samia aliyasema hayo wakati akihutubia kwenye Baraza la Eid el-Fitr jijini Dar es Salaam. Amesema watu wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari kwani virusi vinavyobadilika vinaendelea kuonekana sehemu mbalimbali duniani. Ameongeza kuwa Watanzania takriban 3,950,839 wameshapata chanjo kamili za Corona tangu mwezi Julai mwaka 2021, idadi ambayo inachukua asilimia 13 ya lengo la awali. Amebainisha kuwa serikali itaanza tena kampeni ya kutoa chanjo haraka iwezekanavyo, ambapo inapanga kutoa chanjo kwa asilimia 60 ya watu milioni 60.Wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Jumatano walisisitiza kuwa chanjo bado zina ufanisi mkubwa dhidi ya virusi vya Corona, na takwimu zinaonyesha kuwa kupata chanjo bado kunaweza kuzuia ugonjwa mkali na kifo.