Msomi wa Nigeria: Msimamo wa China kuhimiza amani na mazungumzo kuhusu mgogoro wa Ukraine waitikiwa na nchi nyingi za Afrika
2022-05-05 14:33:05| CRI


Hujambo msikilizaji na karibu katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi hiki cha Daraja msikilizaji kimesheheni mambo mbalimbali yanayohusiana na China na nchi za Afrika, na yanajumuisha sekta mbalimbali za ushirikiano kati ya pande hizo. Licha ya habari, pia tutakuwa na ripoti kuhusu msimamo wa China kuhimiza amani na mazungumzo kuhusu mgogoro wa Ukraine na jinsi ulivyopokelewa vizuri na nchi nyingi za Afrika, pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi yatakayohusu mchango uliotolewa na aliyekuwa rais wa Kenya, Hayati Mwai Kibaki katika ushirikiano kati ya Kenya na China.