WFP yaonya hali ya ukosefu wa chakula yazidi kuwa mbaya katika Afrika Mashariki
2022-05-06 10:11:44| CRI

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa hali ya ukosefu wa chakula inazidi kuwa mbaya katika Afrika Mashariki, ikikadiriwa kuwa watu milioni 81.6 wakiwemo wakimbizi wa ndani na kutoka nje, na jamii za wenyeji katika maeneo ya mijini na vijijini wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula.

Katika taarifa yake WFP imebainisha kuwa hali hiyo inaonesha kuongezeka kwa asilimia 39 kutoka watu milioni 58.6 waliorikodiwa Novemba mwaka 2021, ambapo imechangiwa na ukame, mafuriko, changamoto za kiuchumi na migogoro.

Aidha limesema hali ya lishe katika kanda hiyo ni mbaya, ikikadiriwa watoto milioni 7 walio chini ya miaka mitano wanatarajiwa kuwa na utapiamlo mkubwa katika nchi za Ethiopia, Kenya na Somalia, wakiwemo watoto milioni 1.7 ambao wana utapiamlo mkubwa zaidi.