Viongozi wa juu wa China wasema China itashinda vita dhidi ya UVIKO-19
2022-05-06 10:12:58| CRI

China itashinda vita dhidi ya UVIKO-19 wakati ikiwa na wanasayansi na sera zake za ufanisi za kudhibiti janga ambazo zitastahimili mitahani ya wakati.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Idara ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC ulioongozwa na rais Xi Jinping.

Mkutano huo umechambua hali ya sasa ya kuzuia na kudhibiti Corona, kuangalia vipaumbele na kuweka mipango kwa ajili ya kazi husika. Pia umesema China imekuwa ikihimili changamoto kubwa za UVIKO-19 tangu vita vya kupambana na janga hilo lilipoanza huko Wuhan, na kupata maendeleo kwa juhudi za pamoja za kitaifa.

Mkutano huo ambao umeonya kutozembea katika juhudi za kuzuia janga, umesema wakati virusi bado vinaendelea kuwepo duniani huku vikiendelea kubadilika, kuna wasiwasi mkubwa namna janga litakavyokuwa kubwa zaidi.